Mauzo / POS
Rekodi mauzo kwa taslimu, M-Pesa, benki au deni.
Majibu ya haraka kwa kuweka mfumo, orodha ya bidhaa, wafanyakazi, mauzo bila intaneti, malipo na msaidizi wa AI. Ukikwama, msaada wa WhatsApp upo karibu.
Kuweka mfumo
Weka jina la duka, lugha, na mawasiliano.
Bidhaa
Ongeza kiasi, bei ya kununua, bei ya kuuza na msambazaji.
Mauzo
Rekodi mauzo ya taslimu, M-Pesa, benki au deni kwa simu.
Hatua za AI
Fungua Msaidizi wa AI kuona cha kufanya leo.
Nukuu za Bei
Tengeneza bei za huduma, kazi na bidhaa kabla ya mauzo kuthibitishwa.
Majibu ya haraka kwa kuweka mfumo, orodha ya bidhaa, wafanyakazi, mauzo bila intaneti, malipo na msaidizi wa AI.
Maswali muhimu zaidi ya DukaPilot yapo hapa chini.
DukaPilot
DukaPilot si bei tu. Hizi ndizo sehemu ambazo mfanyabiashara hutumia kila siku: dashibodi, mauzo, bidhaa dukani, madeni, nukuu za bei, maagizo kwa wasambazaji na msaidizi wa AI.

Rekodi mauzo kwa taslimu, M-Pesa, benki au deni.
Ona bidhaa zilizo chini ya kiwango na agiza mapema.
Fuatilia deni la mteja na uweke malipo yakirudi.
Tengeneza agizo na ujumbe tayari kutuma WhatsApp.
Pata hatua za leo: agiza, fuatilia deni, punguza gharama.
Shiriki QR au link; mteja aone bidhaa na atume agizo.
Tengeneza bei za huduma, kazi, vifaa na miradi kabla ya mauzo kuthibitishwa.
Mmiliki anafungua Matawi na kuongeza jina na eneo. Pro inajumuisha maeneo 4 pamoja na duka kuu. Tawi lina bidhaa, mauzo, wateja, madeni, nukuu, wafanyakazi na Daily Close yake. Fungua tawi kwanza kabla ya kuongeza bidhaa au mfanyakazi. Mfanyakazi anaingia kwenye tawi alilopangiwa tu, kulingana na ruhusa zake.
Hamisha bidhaa kati ya matawi kwa kuchagua bidhaa ya kutoka na ya kupokea yenye kipimo na tarehe ya mwisho sawa. Uhamisho si mauzo wala matumizi. Maliza kusawazisha mauzo ya nje ya mtandao kabla ya kubadilisha tawi. Funga Daily Close kabla ya kuhifadhi tawi; rekodi zake hazifutwi.
Usajili na tarehe ya mwisho ni moja kwa biashara nzima. Eneo la ziada ni TZS 10,000 kwa mwezi. Kwenye Malipo, chagua kuongeza matawi hadi usajili uishe au kuongeza mwezi mwingine. Matawi ya ziada hufunguliwa baada ya malipo kuthibitishwa. Hifadhi matawi yaliyozidi kabla ya kupunguza mpango.
Weka jina la duka, lugha, na mawasiliano.
Ongeza kiasi, bei ya kununua, bei ya kuuza na msambazaji.
Rekodi mauzo ya taslimu, M-Pesa, benki au deni kwa simu.
Fungua Msaidizi wa AI kuona cha kufanya leo.
Tengeneza bei za huduma, kazi na bidhaa kabla ya mauzo kuthibitishwa.
Kwa kazi za huduma, miradi, vifaa, labour, transport na amana bila kuharibu stock au ripoti za mauzo.
Hizi huunda namba ya nukuu, mfano QT-0001. Unaweza kutumia {prefix}, {number} na {year}; kila namba lazima ibaki ya kipekee ndani ya duka lako.
Weka siku ambazo nukuu hudumu, sarafu ya kawaida (TZS), na kodi ya kawaida. Unaweza kubadilisha kodi au tarehe kwenye nukuu moja bila kubadilisha default ya duka.
Masharti ya malipo, masharti na vigezo, dokezo kwa mteja, na jina la sahihi hujazwa kiotomatiki kwenye nukuu mpya. Badilisha kwenye nukuu husika pale kazi inahitaji tofauti.
Amua kama mteja aone kiasi, bei kwa kipimo, punguzo la mstari, na vichwa kama Vifaa au Kazi. Hii hubadilisha PDF, print na link ya mteja tu; haionyeshi gharama za ndani.
Weka asilimia ya amana, kwa mfano 50%. Mfumo hukokotoa kiasi kinachotakiwa; malipo halisi huandikwa baadaye kama amana, hatua ya kazi, au malipo ya mwisho.
Tumia portions kwa chakula kinachouzwa na stock ya kawaida yenye barcode kwa vinywaji na bidhaa zilizofungwa.
Pokea kuku mzima, mafuta, mchele, viungo, mkaa na mboga kupitia Pokea Bidhaa. Ukilipa taslimu na shift ya Daily Close iko wazi, malipo hayo hupunguza pesa inayotarajiwa kwenye shift. Usiziweke tena kwenye Matumizi ya kawaida, ili gharama isihesabiwe mara mbili.
Tengeneza Kuku nusu na unit nusu ya kuku, au Wali na kuku na unit plate. Kwa vinywaji tumia bottle, can au glass; barcode inaendelea kufanya kazi kama kawaida.
Fungua Andaa Chakula, chagua ingredients zilizotumika, kisha weka yield iliyotarajiwa na portions halisi zilizotoka. Mfumo unapunguza ingredients na kuongeza portions zilizo tayari kuuzwa.
Ikiwa kuku 10 zilitarajiwa kutoa nusu 20 lakini zimetoka 18, weka 18. Mfumo unaonyesha waste 2 na kugawa gharama yote kwenye nusu 18 halisi. Ongeza gharama kama mkaa au labour kwenye batch na uchague njia ya malipo; taslimu huonekana kwenye Daily Close.
Ukiuza Kuku nusu 1, POS huondoa nusu 1 na kutumia gharama ya batch kwenye faida ya mauzo. Batch zilizohifadhiwa hazihaririwi, hivyo stock history inabaki sahihi.
Lengo si kukuonyesha ripoti tu. Lengo ni kukuambia hatua inayofuata ili duka lisikwame.
Fungua Msaidizi wa AIMauzo, bidhaa, madeni, matumizi, nukuu za bei, maagizo na shughuli za wafanyakazi.
Bidhaa kuisha, deni kukaa muda mrefu, matumizi kupanda, nukuu kuisha muda, au siku bila mauzo.
Kinachoweza kuathiri fedha, faida au uaminifu wa mteja huja kwanza.
Fuatilia deni au amana, agiza bidhaa, punguza gharama, shughulikia agizo, au badilisha nukuu iliyokubaliwa kuwa mauzo.
AzamPesa: Lipa namba 293726045. Selcom: Lipa namba 7006 3589. Jina ni Necuva Group Limited. Weka kumbukumbu ya muamala kwenye Malipo kwa uhakiki. nTZS ikipatikana kwenye Malipo, mmiliki anaweza kuchagua mpango, kuweka simu na kuthibitisha ombi kwenye simu. Usitume PIN hapa. Mpango huwashwa baada ya malipo kuthibitishwa; usilipe tena ikiwa pesa zimekatwa na hali bado inasubiri.
Jisajili, kamilisha duka, ongeza bidhaa chache, kisha rekodi mauzo ya kwanza.
Fungua Orodha ya bidhaa, chagua duka lako, kisha tuma kiungo kwa WhatsApp au mitandao mingine.
Mmiliki anaongeza mfanyakazi, simu na PIN kwenye ukurasa wa Wafanyakazi. Mfanyakazi hutumia simu na PIN kuingia.
Kwenye Pro, mmiliki hutick Kutumia Msaidizi wa AI kwa staff husika. Tick hii haimpei ruhusa ya fedha: cashier haoni faida, madeni, kiasi cha mauzo au matumizi bila ruhusa ya Ripoti.
Ukurasa wa Mauzo unaweza kuhifadhi mauzo kwenye simu bila intaneti na kuyasawazisha intaneti ikirudi. Kagua historia ya usawazishaji kwa hitilafu za kiasi cha bidhaa.
Lipa kwa M-Pesa 52806296, Mix by Yas 18214626, AzamPesa 293726045, au Selcom 7006 3589. Majina ya mpokeaji ni Necuva Group Limited isipokuwa Mix by Yas ni Necuva. Pia unaweza kutuma pesa 0743910580. Hakikisha jina la mpokeaji, kisha weka reference kwenye Malipo au tuma WhatsApp.
Ukurasa wa Malipo unaonyesha maombi yako na hali yake. Msimamizi akithibitisha, mpango utaonekana umeanza.
Anapanga hatua za leo kama kuagiza bidhaa, kufuatilia madeni, kupunguza gharama, kushughulikia maagizo, kufuatilia nukuu inayokaribia kuisha, amana inayochelewa, au nukuu iliyokubaliwa inayosubiri kubadilishwa kuwa mauzo.
Fungua Nukuu za Bei, chagua Nukuu mpya, weka mteja na kazi, kisha ongeza bidhaa za stock au mistari ya huduma, kazi, usafiri na gharama nyingine. Hifadhi rasimu, kagua PDF, halafu tuma link salama kwa mteja.
Hapana. Nukuu ni makadirio tu. Baada ya mteja kukubali, mmiliki huchagua Badilisha kuwa mauzo. Hapo ndipo bidhaa zilizolinkiwa hupunguzwa stock na salio linaweza kurekodiwa kama deni.
Hapana. Gharama za kununua, supplier, markup, faida ya makadirio na dokezo la ndani hubaki kwa biashara. Link, PDF na print ya mteja hutumia taarifa za mteja tu.
Fungua ukurasa wa Delete Account kuona hatua, aina ya data inayofutwa, na muda wa retention.
Bado unahitaji msaada? Tupo tayari kukusaidia kuifanya DukaPilot iwe tayari kwa duka lako.