DukaPilot | Tanzania

Siku ya duka iwe wazi, si ya kubahatisha.

DukaPilot ni mfumo wa simu kwa wamiliki wa maduka na biashara za huduma Tanzania wanaotaka kuona stock, mauzo, madeni, matumizi, pesa ya siku, oda za wateja na nukuu za bei bila kutegemea daftari au kumbukumbu za WhatsApp pekee.

Kiswahili na EnglishSimu kwanzaPesa kwa TZS
Dashibodi halisi ya DukaPilot kwenye simu

Mzunguko wa kila siku

Mfumo unaofuata kazi ya duka.

Hatujajenga ripoti ya kuangalia mwisho wa mwezi tu. DukaPilot inaunganisha maamuzi ya counter, store na owner katika siku yenyewe ya biashara.

Anza na pesa iliyo wazi

Fungua siku ya cash, rekodi mauzo na malipo ya madeni, kisha linganisha pesa ya droo unapofunga siku.

Uza na uache kumbukumbu

Mauzo hubadilisha stock, yanaweka faida kwenye rekodi, na risiti inaweza kushirikiwa kwa WhatsApp, PNG, PDF, au kuchapishwa.

Pokea stock kwa gharama halisi

Weka supplier, invoice, bei ya kununua, usafiri na gharama nyingine. DukaPilot huhifadhi historia ya stock na gharama ya bidhaa.

Geuza link kuwa oda

Shiriki link au QR ya duka lako. Mteja anaona bidhaa na kutuma oda ambayo inaingia moja kwa moja dukani.

Anza kazi kwa nukuu iliyo wazi

Kwa huduma na miradi, tengeneza nukuu yenye kazi, vifaa, labour, amana na masharti. Gharama na faida ya makadirio hubaki ndani ya biashara.

Pesa ya leo iwe na jibu

Daily Close inaonyesha opening cash, mauzo ya cash, makusanyo ya deni, matumizi ya cash, hesabu inayotarajiwa na tofauti ya pesa iliyohesabiwa.

Gharama zisiharibu faida kimya kimya

Ununuzi wa stock huingia kupitia Receive Stock, si matumizi ya kawaida. Hii husaidia buying cost na faida ya bidhaa kubaki sahihi.

Kila mtu aone anachohitaji

Owner anaweza kuweka ruhusa za kuuza, stock, matumizi na reports kwa kila staff. Watu bila Reports hawaoni buying cost au faida ya biashara.

Tulivyojenga

Anza na duka moja, ujifunze kwa kazi halisi.

DukaPilot inaanza vizuri na duka moja, na Pro inasaidia matawi kwa biashara zinazokua. Kila tawi lina stock, mauzo na staff wake; mmiliki anaweza kuhamisha bidhaa na kuona muhtasari wa matawi yote bila kuchanganya rekodi.

Lengo la setup ya kwanza

Bidhaa 10, mauzo 10 halisi, halafu kurudi siku ya pili. Hapo mfumo unaanza kuwa sehemu ya biashara, si app nyingine tu kwenye simu.

DukaPilot

Tuone kama inafaa duka lako.

Tuambie aina ya duka, idadi ya bidhaa na jinsi unavyouza. Tutakusaidia kuanza na setup inayofaa, au kukuonyesha onyesho kwanza.