Futa akaunti yako ya DukaPilot

Ukurasa huu unaeleza jinsi ya kuomba kufuta akaunti yako na data inayohusiana na DukaPilot.

Hatua za kuomba ufutaji

  1. 1Tuma ombi lako kupitia support@dukapilot.com au WhatsApp +255 743 910 580.
  2. 2Tumia nambari ya simu ya akaunti yako ya DukaPilot na jina la duka ili tukuthibitishe.
  3. 3Andika kama unataka kufuta akaunti yote, duka lote, au sehemu fulani ya data.
  4. 4Tutathibitisha ombi na kukamilisha ufutaji ndani ya siku 30, isipokuwa data inayotakiwa kuhifadhiwa kisheria au kwa usalama.

Data inayofutwa

  • Akaunti ya mtumiaji na taarifa za kuingia
  • Taarifa za duka na staff
  • Bidhaa, stock, mauzo, madeni, matumizi na maagizo
  • Catalog ya umma na mipangilio ya duka

Data inayoweza kubaki kwa muda

  • Rekodi ndogo za usalama, audit, malipo, au kodi zinaweza kubaki kwa hadi siku 90 au muda unaohitajika kisheria.
  • Backups za mfumo zinaweza kuchukua hadi siku 90 kusafishwa kikamilifu.
  • Ujumbe uliotumwa kupitia WhatsApp, SMS, email, au huduma za wahusika wengine unaweza kubaki kwenye huduma hizo kulingana na sera zao.

Ufutaji wa sehemu ya data

Unaweza kuomba kufuta baadhi ya data bila kufuta akaunti yote, kama bidhaa, staff, madeni, matumizi, maagizo, au catalog. Tuma ombi hilo kwa support@dukapilot.com au WhatsApp na ueleze data unayotaka ifutwe.